Halmashauri ya Wilaya, imetekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi chini ya Ibara ya 22 inayolenga kujitosheleza kwa chakula, kuimarisha uchumi, kuongeza kipato cha Wakulima, kuwa kichocheo cha kukua kwa viwanda na kuongeza ajira kama ifuatavyo:-
Matumizi ya mbegu bora za mazao ya Mtama, Ulezi, Alizeti, Viazi lishe, Mahindi, Pamba, Korosho na Mihogo yameongezeka kutoka asilimia 30 mwaka 2015 kufikia zaidi ya asilimia 45 mwaka 2019;
Kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara kwa ekari; Mtama kutoka gunia 6 mwaka 2015/2016 hadi gunia 12 mwaka 2019/2020, Mahindi toka gunia 7 mwaka 2015/2016 hadi gunia 13 mwaka 2019/2020, Ulezi toka gunia 8 mwaka 2015/2016 hadi gunia 13 mwaka 2019/2020, Vitunguu toka gunia 10 mwaka 2015/2016 hadi gunia 20 mwaka 2019/2020, Alizeti toka gunia 5 mwaka 2015/2016 hadi gunia 11 mwaka 2019/2020, Viazi vitamu toka gunia 6 mwaka 2015/2016 hadi gunia 10 mwaka 2019/2020. Ongezeko hili ni kwa wakulima wanaotumia mbegu bora na kufuata kanuni bora za kilimo.
Kuongezeka kwa kilimo cha zao la biashara la kudumu la korosho kutoka miti 104,704 mwaka 2015 hadi miti 121,704 mwaka 2019;
Kuongezeka kwa uzalishaji wa zao la pamba kutoka tani 2.2 mwaka 2015 hadi tani 114 mwaka 2019;
Kuongezea mazao thamani hasa kwenye zao la alizeti kwa asilimia 75 na mazao ya mboga kwa asilimia 2.
Kuongezeka kwa uhakika wa chakula katika ngazi ya kaya kwa asilimia 90. Kwa kipindi cha miaka mitano (5) mfululizo hatujawahi kuomba chakula cha msaada.
Kitengo cha Ushirika kimefanikiwa kusajili vyama vinne (4) vya ushirika wa awali (pre-cooperative Societies) ambavyo hujishughulisha na zao la pamba.
Kuongezeka kwa vikundi vilinyojiunga kwenye vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) na Vyama vya Mazao (AMCOS) toka 96 hadi 117 katika kata 10 (Mughunga, Mudida, Ughandi, Ilongero, Kinyeto, Ngimu, Ntonge, Maghojoa, Mtinko na Makuro);
Kusimamia kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wa bodi katika SACCOS 8 na AMCOS 7 kwa kufuata sheria mpya ya vyama vya ushirika ya mwaka 2013.